Bukavu : Mtoto wa umri wa miaka munane azama ndani ya mto Ruzizi

Mto Ruzizi mpaka wa Rwanda n’a DRC.

Duru toka Shirika la raia katani Panzi mtaani Ibanda zaeleza kwamba mwili wa mtoto binti mwenyi umri wa miaka munane umezama ndani ya mto Ruzizi. Mtoto huyo alizama tangu alhamisi tarehe 7 julai 2022. Mwili uligunduliwa na wakaazi wa Ruzizi ya kwanza wa huko Panzi.

Shirika la raia katani Panzi kupitia prezidenti wake Mweresi Redouta Aluta, laeleza kwamba mhanga alizama alipokuwa akifwata mavazi kwenyi mto Ruzizi.

Duru zaongeza kwamba mtoto mwengine aliyekuwa na umri wa mwaka moja na nusu alizama pia mwezi machi uliopita mwaka tunao, alipokuwa akifwata mamae kwenyi mto huwo, pasipo kumkuta.

Shirika la raia katani Panzi laomba wazazi kutoenekana kwenyi mto pamoja n’a watoto wao. Wazazi kushota maji kwa kufanyia usafi nyumbani, kwa kuepuka hatari. Shirika hili laomba pia serkali kuhudumia jamaa mhanga katika sherehe za mazishi. Likiomba mchango wa wote, yaani viongozi wa serkali na wa shirika la raia, ili kupiganisha hatari hiyo, yenyi kusababisha vifo vya watu.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire