Tunaomba raia wenyi kuishi eneo za kanda la maziwa makuu kutoungana na kundi yoyote , hasa yenyi kuchochea ubaguzi na ujeuri. Kwa wenyeji vita, na hata wanaofaidia kupitia vita, kutafuta namna ingine ya suluhu kwa mizozo na kuacha vita, mauaji, wakiwauwa raia wasio na hatia.
Hayo ni miongoni mwa azimio zilizochukuliwa katika kongamano, iliyohitimishwa juma mosi kunako senta Caritas mjini Kinshasa. Mkutano ulioandaliwa na Muungano wa ma Askofu wa Afrika ya kati. Ukijumwisha ma Askofu wa DRC, Rwanda na Burundi. Azimio zilisomwa n’a katibu mkuu wa Muungano huwo Padri Jean Pierre Badiliki.
Pamoja n’a hayo, watumishi wa Mungu waomba wafanya siasa, kuchochea maneno ya ujenzi wa amani na umoja, katika kazi yao.
Viongozi hawo wa kanisa la kikatoliki ,walitowa somo kwa raia wote wa eneo la kanda la maziwa makuu ; » Usiuwe, uwe mchungaji wa ndugu yako. » Ma Askofu hawo watarajiya kuanda kila moja kwenyi diosezi yake misa kuhusu amani na umoja, tarehe 31 julai 2022.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.