DRC : Serkali imekubali ombi kuhusu kuhamishwa kwa jela kuu Munzenze

Jela kuu Munzenze mjini Goma.

Hapa karibuni, jela kuu la Goma Munzenze, litahamishwa. Swala hilo lilikubaliwa na serkali baada ya kuonyeshwa kwa hitaji, naye waziri wa taïfa, akiwa pia waziri wa sheria. Ilikuwa wakati wa kikao cha 61 cha shauri la mawaziri ijumaa iliyopita, mjini Kinshasa.

Jela hiyo nyipya itajengwa kwenyi hekta zaidi ya 15, na litapokea wafungwa 350 elfu. Eneo hilo kutajengwa chumba cha mapumziko kwa wafungwa, uwanja wa michezo, nafasi ya mafunzo kiufundi, shamba na kadhalika hadi jela liweze kujitegemea kama ilivyo kusudiwa ndani ya shauri la mawaziri.

Wana harakati wa Muungano Véranda Mutsanga wanena kufurahiswa na mradi yenyewe. Ila wakumbusha kwamba jela Munzenze ina uwezo wa kupokea wafungwa 150, kwa sasa ni wafungwa zaidi ya elfu 3, ndio wapatikana ndani, na kwamba inabidi kupunguza idadi. Wakiongeza kwamba nafasi ya kujenga jela haijafahamishwa.

Upande wa waziri husika na sheria, pesa zitatafutika ili ya ujenzi wa jela hiyo nyipya, ambayo itaheshimu kanuni ya ujenzi nyipya kimataifa.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire