Pasta Patrick Matei Kimaro kutoka mkoa wa Kilimandjaro nchini Tanzania, alijenga mwenyewe kaburi lake. Anaeleza kwamba anataka wakati atakapoaga dunia, ukoo wake usisumbuliwe na kutafuta pesa za mazishi.
Mtanzania huyo kwa jina maarufu Sabasita, alitayarisha makao yake ya mwisho tarehe 15 januari 2022. Akazaliwa tarehe 2 februari 1963.
Tulipowa hoji watumishi wa Mungu, walionekana kutowa maoni tafauti.
« Patrick Matei Kimaro alikumbuka kwamba aliweza kuzaliwa siku moja, na kwamba atafariki siku moja. Ndiyo sababu ana haki ya kujijengea kaburi nzuri, kutayarisha nafasi mwili wake utakapo lazwa », anena Pasta moja tuliyemhoji.
Ma pasta wengine walisema kwamba kitendo hicho hakikubaliwe kwa kanisa zao.
« Pasta Amini Hangi Prince mchungaji wa kanisa Wokovu,
« Sitasema kibiblia, kama inakubaliwa ama haikubaliwe mtu kujijengea kaburi yake. Kwa sababu watu wengi waongea juu ya Yusufu ambaye anakataa kuzikwa Misri. Akiambia ndugu zake mifupa yake wairudishe kwao watakaporudi. Haiandikwe fasi kama Yusufu alichimba kaburi yake mwenyewe. Halafu huyu ndugu, ikiwa ametayarisha nafasi ya kutia mwili wake, na kusahau nafasi roho itakwenda, atakuwa amekosea. Ni mhimu kama ameandaa nafasi roho itakwenda, kwa sababu mwili haina haja ya mapumziko, ni kitu cha kuoza », afasiria Pasta wa kanisa Wokovu.
Amini Hangi Prince aendelea kujiswali kwa nini mtu kujitengenezea kaburi ijapo ana aina mbili ya wazazi ; wa kimwili na hata wa kiroho. Akiongeza kwamba ni kukosa uaminifu kwa aina hiyo mbili ya wazazi. Na hata akiwa amezaa watoto, kwa nini kujisumbua. Kwake ni uchimbi mtupu.
Kiongozi wa kanisa Wokovu afasiria kuwa kanisa ina jukumu la kutayarisha roho ya mtu mbele ya kufariki. Na baadae hutengeneza mwili wake pamoja na nafasi utalazwa kwenyi makao ya mwisho.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.