Asia/ Sri Lanka: Raia wa nchi hiyo walazimisha Raisi wao na waziri mkuu kujiuzulu wakiwashutumu uongozi mubaya

Maelfu ya raia wa Sri Lanka wakivamia makao ya Raisi wao.

Ni tangu siku kadhaa, maelfu ya waandamanaji wa Sri Lanka wamepiga goti kwenyi makao ya Raisi wao Gotabaya Rajapaksa na ya waziri mkuu, wakiwa wenyi hasira kutokana na kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo.

Wakati Raisi Gotabaya Rajapaksa anatarajiya kujiuzulu rasmi juma tano, waandamanaji wanapinga serkali inayojumwisha vyama vyote vya kisiasa, wakisema itatowa nafasi kwa familia ya Rajapaksa.

Raia wa Sri Lanka ndani ya makao ya Raisi Gotabaya Rajapaksa.

Duru toka nchi ya Sri Lanka zaeleza kwamba wengi wa waandamanaji hawataki chama cha Sri Lanka, kinacho zibitiwa na familia Rajapaksa, kubaki madarakani. Hawataki chama cha Raisi huyo kuwa sehemu ya serkali ya vyama vyote.

Tufahamishe kwamba waandamanaji hawo wanasema hawatatoka kwenyi majengo ya serkali, hadi pale Raisi na waziri mkuu watakapo uzulu rasmi.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire