Goma : Chama cha kisiasa ; Ensemble pour la République ni suluhu kwa shida za wakongomani kwa jumla na mashariki mwa DRC kwa peke( Promesse Matofali)

Akiwasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii juma nne tarehe 12 julai 2022, Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Promesse Matofali anena kuwa mwenyi furaha akihubiri habari njema. Ni kutoka chama cha kisiasa Ensemble pour la République ili ya kupata suluhu kwa shida ya wakongomani.

«  Ujumbe ni kwamba chama « Ensemble pour la République’, kinakuja kuleta suluhu kwa shida tulizozikuta mahali tunatoka na kote nchini DRC. Tuliweza kwambia raia kwamba, tangu uhuru wa nchi hadi sasa, hatujawai kupata viongozi wenyi mpangilio wa kazi. Na ndio maana, tulijaribu kufasiria raia maana ya Chama Ensemble pour la République. Kwa nini kimeundwa, tofauti kati ya chama hicho na vyama vingine. Mwishowe kuhusu Prezidenti wa chama Moïse Katumbi Tchapwe ambaye ni mfano wa kuiga, aleza Mwanabunge Promesse Matofali.

Mbele ya yote aligusia hali mbovu ambamo aliwakuta raïa wa Béni, Lubero, Oicha na penginepo ambako alitembelea.

« Gunia ya saruji ni dola 18 za marekani, litri moja ya petroli ni franka elfu 5 za Kongo. Watu hawafike kwenyi shamba zao. Kwa jumla hali ya kutishia afasiria« , kwa huzuni Mwanabunge Promesse Matofali.

Kuhusu kupunguzwa kwa mapashwa ya uongozi wa kijeshi jimboni Kivu ya kaskazini, Promesse Matofali anena kuwa ni jambo alilolitamka mbeleni. Kwa kuwa uongozi wa kijeshi ulihusika na operesheni za vita pamoja uongozi wa jimbo. Na hiyo ilipelekea kutofaulu.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire