Kivu ya kaskazini/ Nyiragongo: Raia watowa malalamiko kuhusu uhaba wa maji safi eneo hilo

Territoire de Nyiragongo.

Raia wilayani Nyiragongo watowa malalamiko kuhusu uhaba wa maji safi makwao. Hasa kwenyi vijiji vingi vya Buhumba na Kibati wilayani Nyiragongo.

Tangu shirika husika na maji safi Regideso lili arifu raia kukatwa kwa maji kwa muda, wakaji hawo hawajaona toni kutiririka ndani ya mirija.

Bosenibamwe Muzungu memba wa shirika la raia wilayani Nyiragongo anena kuhuzunishwa na hali ambayo husumbua raia. Huyu asema wengi huamka usiku wakienda kwa mlolongo kutafuta maji.

Mwanamemba huyo wa shirika la raia asikitika kuona raia wengi huenda kutafuta maji kwenyi tanki, ijapo vinyume kutoka maji hiyo ambayo si safi. Kwa hiyo jerekani moja iliyo nunuliwa franka za Kongo 100, kwa sasa ni franka 200 za Kongo.

« Tunaomba mashirika zisizo za kiserkali kutuletea maji safi kwa kuwa tunateswa sana. Hasa wakati huu wa ugonjwa wa korona, unaoshurtisha kutumia maji kila mara , anena Bosenibamwe Muzungu.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire