RDC : Mwanabunge Jean Baptiste Kasekwa aomba iundwe kamisheni ya uchunguzi wa kazi za pamoja UPDF FARDC

Mwanabunge Jean Baptiste Kasekwa

Mwanabunge wa taïfa Jean Baptiste Kasekwa mchaguliwa wa Goma asisitiza kuunda kamisheni ya uchunguzi ya pamoja, ili kuzungumzia swala na kuazibu wote wanaokwamisha amani kwenyi mapambano. Akiarifu kwamba njama zafanyika kuhusu DRC, na ukosefu wa uwaminifu kati ya raia na jeshi la taïfa.

Jean Baptiste Kasekwa alijibu kwenyi vyombo vya habari mjini Kinshasa. Akihojiwa kuhusu kwendelea ama la kwa operesheni za pamoja UPDF FARDC, ijapo kuongezeka kwa vitendo vya ujeuri, na shambulizi kila leo ya raia na waasi wa ADF.

 » Natowa angalisho kwa serkali na wakongomani wote kwa jumla, kwamba dalili zaonyesha kuwa kuna njama zenyi kuhatarisha amani DRC sawa hali tunayoishi leo wilayani Rutshuru. Je tuendelee na operesheni za pamoja UPDF FARDC hadi sasa? Kumeonekana ukosefu wa matumaini kati ya pande hizo mbili FARDC na UPDF. Ndio maana naomba iundwe kamisheni ya uchunguzi ya kweli, asisitiza Jean Baptiste Kasekwa.

Mwanabunge huyu aongeza kwamba alijielekeza mjini Béni ambako alikutana na ma ofisa wa UPDF. Wakimwambia kwamba kuna shida ya ndani, wenyewe kwa wenyewe, jambo lenyi kukwamisha kazi.

« Raia nawo hubebesha mzigo kwa pande zote mbili, jambo halieleweki. Mbele ya kuendelesha operesheni hizo, inabidi kuunda kamisheni ya uchunguzi ya pamoja, yaani jeshi, serkali pamoja na wabunge na shirika la raia. Katika lengo la kuchunguza mwenendo wa kazi na kujuwa jukumu la kila moja, na kuazibu wahusika. Kama sivyo, jeshi litaendelea pasipo kufaulu hadi mwisho, anena Jean Baptiste Kasekwa.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire