DRC : Inabidi kuboresha kazi za jeshi ili kukomesha vita nchini hususan mashariki mwa DRC ( Julien Paluku Kahongya)

Waziri husika na viwanda nchini DRC Julien Paluku Kahongya.

Waziri husika na viwanda nchini DRC, Julien Paluku Kahongya anena kwamba makubaliano ya amani hailete suluhu kati ya serkali ya DRC na waasi wa M23. Siyo njia kwa kutanzua mizozo aina ya M23.

Alinena hayo juma nne tarehe 12 julai alipohojiwa na wandishi habari katika kipindi Dialogue entre congolais kwenyi redio Okapi.

« Nazani kwamba makubaliano ya amani ni alama ya kushindwa kwa jeshi, ndani ya nchi. Nchi zinazo jiandaa ipasavyo hazijihusishe na makubaliano ya amani. Kila mara, nakumbusha jambo hilo, na hata nilipokuwa liwali. Nazani kwamba DRC yapashwa kuboresha kazi za widhara ya ulinzi. Muliweza pia kufwata Raisi wa DRC, katika hotuba yake ya tarehe 30 juni. Akitowa mwito kwa vijana, ili kujiorodhesha jeshini. Kwa kuwa aligunduwa shida. Hakiba yetu ni kuboresha sekta ya ulinzi. Kwani makubaliano ya amani kila leo ni alama ya kushindwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Ni tangu awali, tulianza sahini makubaliano ya amani, pasipo suluhu, anena aliyekuwa liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini.

Upande wake Profesa Bob Kabamba, mwalimu kwenyi univasti ya Liège huko Brussels, ingawa jeshi FARDC halijafaulu vita dhidi ya waasi wa M23 pa Bunagana, ni kwamba jeshi hilo lapigana na kundi mbili. Nazo ni wanajeshi wa Rwanda na wa Uganda.

« Hali tunayo kwa sasa, yawezekana jeshi la taïfa lishindwe kufukuza waasi M23 pa Bunagana. Sababu ni kwamba Rwanda inaunga mkono waasi hawo, hata na Uganda. Swala, kwa nini Uganda pia. Ijapo nchi hiyo yasaisia FARDC kwa kugonga ADF, upande wa kaskazini. Pia ripoti toka shirika la raia zataja jeshi la Uganda kujiingiza ndani ya mizozo upande wa waasi wa M23, tukiwa kusini. Hali hiyo yapelekea FARDC kushindwa kufukuza waasi wa M23 pa Bunagana na kando yake, mahali wanapo zibiti kwa sasa, afasiria Bob Kabamba mwalimu mkuu kwenyi univasti.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire