Kinshasa : Asilimia chini ya tano ya waganga yapokea chanjo dhidi ya virusi vya Ebola

Habari toka mjini Kinshasa zaeleza kwamba Uratibu husika na chanjo dhidi ya Ebola nchini DRC, yaandaa kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo. Imeonekana mwanzoni mwa kampeni hiyo, kwamba asilimia chini ya tano ya waganga yapokea chanjo dhidi ya virusi vya Ebola.

Kwa kupata suluhu kuhusu jambo hilo, vikao kadhaa vimeandaliwa ajili ya waganga, wakifunzwa umuhimu wa kupokea chanjo.

Duru zetu toka Kinshasa zaeleza kwamba kumeandaliwa kikao ki elimu. Ni katika lengo la kufasiria umuhimu wa kupokea chanjo dhidi ya virusi vya Ebola. Na ni muda wa kuendesha haraka chanjo dhidi ya virusi vya Ebola.

Uratibu husika na chanjo dhidi ya virusi vya Ebola nchini DRC ulionyesha pia kwamba waganga kama vile watu wengine hawakuweza kuhamishwa vilivyo dhidi ya ugonjwa wa korona.

Baada ya kikao, washiriki wameahidi kuhamisha wengine kuhusu umuhimu wa chanjo dhidi ya virusi hivyo.

Tukumbushe kwamba, tangu mwanzoni mwa ugonjwa huo, watalaam wa afya walichagua aina mbili ya watu wenyi kustahili chanzo mbele ya wengine, wakitaja waganga na watu wenyi umri wa miaka 55 na zaidi.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire