DRC : Waziri wa taïfa husika na mambo ya kazi Claudine Ndusi yupo ziarani jimboni Kivu ya kaskazini na kusini ili kuchunguza kazi

Waziri husika na mambo ya kazi Claudine Ndusi kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma.

Waziri husika na mambo ya kazi Claudine Ndusi amewasili hii alhamisi tarehe 14 julai mjini Goma, ili kuchunguza hali ya kazi ndani ya sekta yake.

Akihojiwa n’a wandishi habari, Bi Claudine Ndusi anena kuja Kivu ya kaskazini na kusini, kuchunguza jisi kazi zafanyika ndani ya majimbo hayo. Pamoja n’a hayo, namna gani yaendeshwa mafunzo ya kiufundi, ajili ya kuwasindikiza askari jeshi walio weka chini silaha.

« Nafanya safari ili ya kujioneya binafsi gisi kazi zafanyika ndani ya sekta yangu. Nimependa kuanza na jimbo la Kivu ya kaskazini, mbele ya kwenda kusini. Hiyo ni kulingana na hali ya mambo. Kumbukeni pia kwamba twafanya mafunzo kiufundi ili kuwasindikiza askari jeshi walio weka chini silaha, na wengine wote wenyi kuhitaji waingie ndani ya maisha ya kawaida,« anena waziri Bi Claudine Ndusi.

Akiongeza kwamba atajihusisha na swala la kuunda kazi kwa vijana. Tukumbushe kwamba baada ya Goma, atajielekeza mjini Bukavu, katika lengo lile.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire