Goma: Acheni Lukwebo aomba raia kupokea kwa shangwe na vigelegele Prezidenti wa seneti nchini DRC

Akiwa njiani kuhusu likizo, Prezidenti wa seneti nchini DRC, Modeste Bahati Lukwebo atawasili hii ijumaa tarehe 15 julai mbele ya kwenda mjini Bukavu eneo alilochaguliwa.

Acheni Lukwebo, mratibu wa shirika FONDALU, akiwa ndani ya timu lililo tangulia, aalika raia kupokea Prezidenti wa seneti nchini DRC Modeste Bahati Lukwebo kwa shamra shamra ambaye atawasili hii ijumaa tarehe 15 julai mjini Goma. Baadae kujielekeza mjini Bukavu jimboni Kivu ya kusini.

Akihojiwa kuhusu usalama mashariki mwa DRC, Acheni Lukwebo alitowa mbele ya yote pôle kwa raia wenyi kukumbwa na usalama mdogo eneo hilo.

Tufahamishe kwamba shirika FONDALU, lahusika na swala za kijamii na kiutamaduni, maendeleo, maisha bora kwa wakongomani, umoja wa makabila Kivu ya kaskazini na kusini na hâta kwa nchi nzima.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire