Goma: Prezidenti wa seneti Modeste Bahati Lukwebo asisitiza kurudi kwa vikosi vya MONUSCO kwani vimeshindwa kazi na kusindikiza Raisi Félix Antoine Tshisekedi kwa mhula mwengine

Mimi na ujumbe inayo nisindikiza tulikuja kwanza,  hamasisha vijana waingie jeshini, ili wapiganie udongo wa nchi yao, îli kutekeleza amani ya kudumu. Tutashinda vita, tunapashwa shinda hii vita isiyo halali. Namna gani vikosi vya MONUSCO hapo awali MONUC ambavyo ni watu elfu ishirini wapo kwenyi udongo wa DRC, miaka ishirini na mbili sasa, ila vita vyaendelea. Watu hawo warudi kwao.  Inabidi tujitegemee wenyewe, tujipiganie sisi wenyewe.

Prézidenti wa seneti Modeste Bahati Lukwebo alinena hayo alipowasili mjini Goma toka mji mkuu Kinshasa. Alijielekeza kuja kwenyi likizo jimboni Kivu ya kusini, ambako ni mchaguliwa.

« Huyu aliangazia raia kwamba jumhuia ya kimataifa imekwisha onyesha unjanja kwa kukatalia iDRC kununua silaha, ili kushinda vita. Sisi tutatumia silaha yoyote île tunayo , maana nguvu za raia zinashinda hata silaha. Tujisumbukie wenyewe kwa wenyewe, » aeleza Bahati Lukwebo Prezidenti wa seneti nchini DRC.

Prezidenti wa seneti alifahamisha pia  kwamba DRC yataka uhusiano kila mara na nchi jirani, ijapo nchi hizo kuchokoza DRC. Ingawa nchi hizo zinahitaji uhusiano, na kazi nchini, inabidi ziongee  na DRC, inabidi ikuwe kwa faida ya pande zote mbili.

Akishukuru Mungu anayetulinda kila saa na kila dakika,  Modeste Bahati Lukwebo alifahamisha umuhimu wa kuunga mkono Raisi wa DRC Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo kwa muhula mwengine. Ili aweze kufaulu kutekeleza usalama na maendeleo nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire