Ilianzishwa hii tarehe 18 julai 2022 mtihani wa serkali kwa wanafunzi wa shule la sita la sekondari kote nchini DRC. Mwanabunge wa taïfa Ayobangira Safari mchaguliwa wa Masisi atakia wanafunzi hao kufaulu kwa mashindano ya kuhitimisha elimu ya sekondari.
« Tunatumaini mara haba kwamba mwaka huu watoto watasoma vizuri, hasa wale waishio eneo za mizozo. Tuna wanafunzi wilayani Rutshuru, ambao walikimbia vita nchini Uganda. Viongozi wa kijeshi na wa kiraia wafanya iwezekanayo, ili watoto hawo wafanye mtihani, kama ilivyo wakati wa mtihani wa shule la sita la msinji yaani ENAFEP, anena Mwanabunge Ayobangira Safari.
Mchaguliwa wa Masisi azani kwamba wanafunzi wenyi kupatikana eneo za mizozo, mfano wa Masisi upande wa Bashali watafaulu kufanya mtihani.
« Kama, ilivyo desturi, twatowa msaada kwa wanafunzi waliofaulu zaidi, na hâta kwa wenyi shida kijamii. Mwaka huu, kuhusu msaada kijamii, tutageukia upande wa wanafunzi waliokimbia vita nchini Uganda. Hata na wenyi kupatikana pa Pinga wako miongoni mwa watatolewa msaada kijamii. Na wengine wote mutajulishwa wakati wa kutangaza matokeo ya mtihani, aeleza Mwanabunge Ayobangira Safari.
Akihojiwa kuhusu nafasi atakazo zitembelea wakati huu wa mtihani, Mwanabunge Ayobangira anena kwamba, waliweza kutembelea wilayani Rutshuru wakati wa mtihani wa shule la sita la msinji. Akiongeza kwamba kuna timu kubwa huko Rutshuru, ambalo litafanya mzunguko, ili kuchunguza kazi.
Kuhusu usalama wilayani Masisi, Mwanabunge huyu anena kwamba hakuna usalama, kwani vita vyaendelea. Akisisitiza kwamba ni kutokana na ukosefu wa idadi ya askari jeshi FARDC. Pamoja n’a hayo, kupelekwa kwa askari jeshi kwenyi eneo za mapigano Rutshuru, Béni , kutoka eneo zingine. Pia kuchelewa kwa serkali kuwaingiza vijana walioondoka jeshini ndani ya maisha ya kawaida, maana vijana waliosababisha usalama mdogo huko Pâti , ni wenyi kungojea waingizwe ndani ya maisha ya kawaida na serkali.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.