Kivu ya kaskazini/Nyiragongo : Wanafunzi 250 na wazazi wao wa EPST 2 Kibumba/ Buhumba ya kwanza washukuru Mwanabunge Mwanza Nangunia kwa kuwalipia pesa kuhusu mtihani

Bwana Bosenibamwe Muzungu wa shirika lisilo la kiserkali ACADEPA ZABURI 133 anena kwamba wazazi wa wanafunzi wa EPST Nyiragongo 2 Kibumba na Buhumba washukuru Mwanabunge wa taïfa Mwanza Nangunia. Ambaye aligusa ndani mfuko ili wanafunzi hawo 250 wafanye mtihani wa kuhitimisha shule la nane la sekondari.

Alifahamisha hayo akihojiwa na ripota wa la ronde info wiki hii mjini Goma.

Bosenibamwe Muzungu wa shirika ACADEPA ZABURI 133, anena kwamba, kuna wanafunzi wengine wenyi kungojea mtihani wa serkali wa shule la sita la sekondari, na hawana msaada wowote ule.
Akiomba Mwanabunge huyo, serkali mashirika zisizo za kiserkali, ama mtu mwengine wa moyo mwema, kuwasaidia, ili wafanye mtihani. Kwani wana woga kutofanya mtihani huo.

Tunakumbusha kwamba mtihani wa serkali wa shule la sita la sekondari ulianza hii juma tatu tarehe 18 hadi tarehe 21 julai 2022.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire