Kivu ya kaskazini : Wafanya byashara wa Butembo na Lubero waacha mgomo na kurudilia kazi

Wafanya byashara jimboni Kivu ya kaskazini wameacha mgomo, wakianza kubeba na kuleta bidhaa kupitia mipaka ya Kasindi , Lubiriya wilayani Beni.

Hatua hiyo ilichukuliwa ikiweko ujumbe toka serkali Kivu ya kaskazini, ilioongozwa na mshauri wa liwali husika na mambo ya pesa, pamoja n’a wafanya byashara wa Butembo, Lubero FEC maarufu kwa kimombo.

Kikao ilifanyika ndani ya jumba la mea wa Butembo hii juma tano tarehe 20 julai 2022.

Mjumbe wa liwali David Kamugha alifurahi kuona wafanya byashara kusimamisha mgomo na kurudilia kazi. Akiwaahidi kukinga byashara yao. Miongoni mwa walioshiriki kikao, madreva, watumishi mipakani na kadhalika.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire