Prezidenti wa chama cha kisiasa AFDC Modeste Bahati Lukwebo ameanzisha rasmi juma nne tarehe 19 julai 2022, semina ya mafunzo dhidi ya wanamemba wa chama AFDC, husika na mawasiliano.
Wakati huo, Modeste Bahati Lukwebo aomba washiriki semina kutia mkazo kwa yale wanayofunzwa, na kuitekeleza.
» Ndani ya kazi zote, mawasiliano ni mhimu sana, ukiwasiliana vibaya, shirika lako litatoweka. Tulianza mjini Kinshasa, ni muda wa jimbo la kaskazini na kusini, tutaendelea hata kwenyi wanamemba wa chama huko ugenini. Ili wenyi kupokea mafunzo haya wapate ujuzi. Chama AFDC na hata Muungano wetu, tutasindikiza Raisi wetu Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo kwenyi uchaguzi wa mwaka 2023, »/ aeleza Prezidenti wa seneti Modeste Bahati Lukwebo.
Akiongeza kwamba mafunzo hayo yatafanyika ndani ya majimbo kote nchini DRC, ili kuinua chama AFDC.
Tufahamishe kwamba semina hiyo inahusu siasa na historia ya chama AFDC, nafasi ya mawasiliano kwa sasa ndani ya chama, pamoja n’a matumizi ya vyombo vya mawasiliano vya kisiasa.
Watalaam wa walimu toka hapa na pale wanahudumia semina hiyo.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.