Gari, pikipiki, wapita njia walionekana wengi barabarani hii alhamisi tarehe 28 julai 2022 mjini Goma. Ni baada ya mituto ya risasi iliyo pelelekea vifo vya watu yapata kumi na tano na zaidi ya wengine sitini kujeruhiwa vikali. Ikiwa ripoti kutoka mnenaji wa serkali ya DRC Patrick Muyaya.
Wandishi habari wa la ronde info walifanya mzunguko mjini Goma. Kwenyi soko la Birere, wachuuzi walionekana wengi nafasi zao za byashara, wakizungukwa na wateja. Kwenyi barabara kubwa za mji, gari, pikipiki, na wapita njia walionekana wengi. Kwenyi uwanja wa ndege, hali ni kama kawaida. Wasifiri wakienda na wengine wakirudi
Hakuna milio ya risasi ilisikika tangu asubui hadi jioni hii alhamisi tarehe 28 julai, kama ilivyo kuwa siku tatu za mbeleni. Pamoja na hayo, mawe zilizowekwa hapa na pale barabarani tayari zimeondoshwa. Vijana wenyi hasira walionekana kunyatuka zao.
Tufahamishe kwamba hali ilirudi tulivu, baada ya viongozi wa serkali nchini DRC kuomba raia waweke silaha chini dhidi ya MONUSCO. Walitowa ujumbe wa rambi rambi kwa jamaa zilizo poteza watu ndani ya machafuko. Wakisema kuwa wamesikia malalamiko ya raia.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.