Liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini Jenerali Constant Ndima ameahidi ma mia ya vijana walio ondoka ndani ya kundi zenyi kumiliki silaha, kufikisha malalamiko yao kwenyi tabaka za juu. Ni vijana wenyi kupatikana ndani ya kempi ya Mubambiro karibu miaka tano sasa, wakingojea huduma ya serkali.
« Kuvumilia mingi inaleta uchungu na hata matunda mazuri. Serkali inafahamu kama munapatikana mahali hapa, Hata kama muliweza ingia ndani ya kundi zenyi kumiliki silaha, Mulijibu kwa mwaliko wa Raisi kwa kuwa munapenda nchi yenu . Ndio maana inabidi tutembee pôle pôle ili tufikie mambo mazuri. Hii ndio sababu ya kushimama kwetu mahali hapa. Gisi mulikuja kwenyi mlolongo na kufika hapa na ndivyo tutarudi pamoja hadi kwenyi kempi yenu ambako mutapata suluhu. Mimi ni baba yenu nikiwa liwali na ndo maana wa mama na watoto wote turudi kwenyi kempi mahali mulitoka », asisitiza liwali wa jimbo Constant Ndima.
Aliendelea kuomba vijana hawa walio weka silaha chini warudi wapate chakula, kwa kuwa serkali kwa jumla inafahamu kwamba wapatikana mahali hapo. Na kwamba suluhu itapatikana.
Mwakilishi wa vijana Bwana ASSANI alisema kufurahi kuona serkali ingali nafahamu kwamba wapatikana mahali hapo.
« Hatuku toka ndani ya kempi ya Mubambiro kuja kuunda kempi ingine mahali hapa. Ama hatuku kuja kwa kutafuta kuunda njama. Malalamiko yetu ni moja: Tunaishi ndani ya kempi tukiwa na bibi zetu na watoto katika hali mbovu ya maisha. Miaka tano sasa. Tunaomba shirika PDDRCS lililo tupokonya silaha na kutupa kadi ya raia, litulipe pesa zetu za kuturudisha ndani ya jamaa, Watoto wapate kusoma na wa bibi wafanye shuguli zao. Nasi tunakuwa na jukumu ndani ya jamaa zetu, » anena Bwana ASSANI akiwa mbele ya liwali.
Mara tena liwali aliahidi kufikisha malalamiko kwa shirika PDDRCS, na kwa serkali nzima. Aliahidi pia suluhu kwa muda kwa ngambo yake, kwa kungojea suluhu la kudumu kwenyi ngazi za juu mjini Kinshasa. Baadae akawagawanyia chakula na kinywaji mbele ya kurudi kwenyi kempi pa Mubambiro.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.