Kivu ya kaskazini ; Kuandamana kwa raia isiwe msinji ya vitendo vya ujeuri ( Profesa Daktari Joseph Kitaganya)

Akihojiwa na mwandishi habari wa la ronde info hii alhamisi tarehe 28 julai, Profesa Daktari Joseph Kitaganya alaumu Pia vitendo vya ujeuri wakati wa maandamano. Kuandamana ni haki ya raia ili siyo msinji wa kuchoma gurudumu barabarani, kupora mali ya watu, kutupa mawe na vitendo vingine vya kinyama.

« Raisi wa DRC, Prezidenti wa seneti pamoja na spika wa serkali wanalaumu vitendo vya ujeuri vilivyo tendeka wakati wa maandamano. Yaani uporaji, kuchoma gurudumu, vifo vya watu, kutupa mawe na kadhalika. Nazani kwamba siyo namna nzuri ya Kuandamana.  Raisi wa DRC amenena kwamba MONUSCO ni mshirika wake. Kwa kuwa wamejionea wenyewe machafuko iliyo tendeka humu jimboni, nazani Raisi wa nchi ataomba shauri la umoja wa mataifa kuondowa vikosi vyake nchini DRC, » afasiria Profesa Kitaganya.

Kutokana na Daktari Joseph Kitaganya; « viongozi wa serkali yaani Prezidenti wa seneti na wengineo hawawezi kutuma raia kufanya machafuko. Inabidi raia wasubiri kwa kungojea jibu toka viongozi wa serkali. Kwani udemokrasia  ni sauti ya raia, kwa manufaa yao wenyewe », anena kiongozi huu wzamani wa chuo kikuu ISC.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire