Kivu ya kaskazini : Profesa Daktari Joseph Kitaganya aomba raia kuepuka vitendo vya ujeuri wakati wa maandamano, wakiheshimu sheria

Profesa Daktari Joseph Kitaganya

Akihojiwa na mwandishi habari wa la ronde info, hii ijumaa tarehe 28 julai 2022, Profesa Daktari Joseph Kitaganya aomba raia kuepuka vitendo vya kinyama, wakati wa maandamano. Wanapotowa malalamiko yao kwa serkali, ambayo ina jukumu la kutafuta suluhu kwa shida zao.

Alinena hayo kulingana na hali ya machafuko iliyopitika siku hizi mjini Goma. Raia wakilazimisha vikosi vya MONUSCO viondoke kwenyi ardhi ya DRC. Kwa kuwa vimeonekana kushindwa kutekeleza usalama, miaka zaidi ya ishirini sasa.

« Viongozi wa serkali yaani Raisi wa DRC, Prezidenti wa seneti pamoja na spika wa serkali wamelaumu vitendo vya ujeuri, vilivyo sababisha vifo vya watu, uporaji, kuharibu jengo hapa na pale. Maandamano siyo msinji ya vitendo vya wizi, vya uporaji, vya kuchoma gurudumu barabarani na kadhalika. Raisi wa nchi alieleza kwamba MONUSCO ni mshirika wake. Huyu ana jukumu la kuomba shauri la usalama la umoja wa kimataifa kurudisha  vikosi vya MONUSCO nchini mwao. Kwa kuwa udemokrasia ni kauli ya raia kwa manufaa yao wenyewe, » anena mwalimu mkuu Kitaganya.

Tukumbushe kwamba raia wenyi hasira kali waliandamana mwanzoni mwa wiki, wakilazimisha  vikosi vya MONUSCO kurudi makwao. Jambo lilizo zusha kasoro mjini Goma, na kupelekea vifo upande wa raia na hata upande wa MONUSCO.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire