Tujiunge pamoja kwa kuweka viongozi wa nchi wenyi kutu heshimu na kufanya matakwa yetu. Viongozi wa nchi wachukuwe jukumu lao, wakiheshimu katiba ya nchi na hâta sheria ,husika na ukingo wa watetezi wa haki ya binaadam jimboni Kivu ya kaskazini.
Matamshi ni yake Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Promesse Matofali, akionyesha huzuni kuhusu kuwasambaza mara tena waandamanaji, walio kuwa kwenyi makesha kunako mashanganjia VGH mjini Butembo. Hawa wakingojea kufanya mazishi ya ndugu zao, walijikuta kusambazwa na vyombo vya usalama. Jeneza nane zilipelekwa mahali pasipo Julikana.
Promesse Matofali azani mara tena kujitokeza kwa vifo na majeraha katika kusambazwa kwa raia hawa na vyombo vya usalama. Raia walikuwa kwenyi makesha wakilia ndugu zao. Wakijuta kuhusu serkali ya DRC na mshirika wake, ambao hawakufaulu kukomesha mauwaji na kutekeleza usalama nchini.
Mwanabunge huyu aangazia kwamba kitendo hicho cha kinyama ni ukiukaji wa kipengele cha 26 cha katiba ya nchi. Kipengele hiki kinawapa uhuru waandamanaji, ijapo kutoheshimu kwa serkali.
Promesse Matofali aongeza kwamba kila mara hukumbusha kazi ya vyombo vya usalama yaani kulinda raia na mali yao.
« Kila mara vyombo vya usalama huonyesha nguvu dhidi ya raia wasio na ulinzi na walio poteza mengi katika mauwaji ya alaiki na usalama mdogo wa kila aina, » Hâta serkali kupinga watu kuzika ndugu zao, watu kufanya mazishi kwa uficho, bila jamaa za wahanga kulia ndugu zao, » anena Mwanabunge Promesse Matofali.
Akihitimisha kwa kutowa ujumbe wa rambi rambi kwa jamaa zote zenyi kuangamizwa na hasa kukumbwa na misiba jimboni Kivu ya kaskazini.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.