Kivu ya kaskazini : Shambulizi la ADF barabara Kasindi Béni lapelekea vifo na majeraha

Waasi wa ADF walishambulia hii ijumaa tarehe 29 julai 2022 Lori moja aina DYNA kwenyi barabara Kasindi Béni. Hapo hapo mtu moja alifariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa vikali.

Prezidenti wa shirika la raia tawi ndogo la Rwenzori Mulala ahakikisha kwamba gari hiyo ilikuwa ikitokea pa Kasindi na kujielekeza mjini Béni.

Upande wake kamanda wa operesheni Sokola1, luteni Anthony Mwalushay anena kwamba gari iliyo anguka ndani ya mtego wa wajangili ADF, haikuweza kubali kungoja safari ya kusindikizwa ndani ya mlolongo. Na ndivyo iliweza kunaswa na wanamugambo ADF.

« Kuna gari moja aina DYNA ambayo haikupenda kuheshimu kanuni zetu za usalama. Gari hiyo ilienda peke. Ilipofika kwenyi barabara Nyaleke na kilalo Semliki ikaanguka ndani ya mtego wa waasi ADF,, »afahamisha kama Anthony Mwalushay.

Tufahamishe kwamba shambulizi hilo ni mara ya kwanza , tangu wafanya biashara wa Butembo Béni walianza mara tena kutumia barabara yenyewe. Siku zilizo pita waliweza kusimamisha kazi kutokana na usalama mdogo kwenyi barabara hiyo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire