Kivu ya kaskazini : Vikosi vya MONUSCO vilivyo fyatuwa risasi dhidi ya raia na kusababisha vifo na majeraha mipakani Kasindi , vimewekwa korokoroni

Katika tangazo lake hii juma pili tarehe 31 julai 2022, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa kimataifa Bi Bintou Keita asema kuwa na huzuni. Ni kutokana na kufyatuwa risasi kwa vikosi vya MONUSCO dhidi ya raia, ambayo ilipelekea vifo na majeraha. Hayo yalifanyika kwenyi mpaka pa Kasindi kati ya DRC na Uganda.

Bi Bintou Keita anena kwamba vikosi hivyo vya MONUSCO vilikuwa vikitoka likizoni. Wakati mpaka wa Kasindi imefungwa, Waandamanaji wakiweka vizuizi kwa kuwa hawataki tena MONUSCO nchini. Ndipo vikosi hivyo vilivyatuwa risasi na kusababisha vifo na majeraha.

« Tumegunduwa askari walio sababisha ajali hiyo na tumewa weka korokoroni. Kwa kungojea uchaguzi ambao tayari umeanza, pamoja na serkali ya DRC, nchi zao walikotokea, jamaa za wahanga na hâta washahidi ili wahusika waazibiwe vilivyo, » anena Bi Bintou Keita.

Kwa ukumbusho ni karibuni wiki moja, tangu raia jimboni Kivu ya kaskazini, waliandaa kampeni ili MONUSCO aondoke nchini DRC, kwa kuwa hakufaulu kutekeleza amani. Maandamano yalipelekea mara tena vifo na majeraha pande mbili husika.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire