Bukavu : Ajali ya barabarani imefanyika pa Feu vert katani Nguba mtaani Ibanda

Upande moja ya mtaa wa Ibanda

Ajali ya barabarani imejitokeza hii juma pili tarehe 31 julai 2022 kwenyi nafasi Feu vert pa Nguba mtaani Ibanda, na kusababisha majeraha. Hayo yalifanyika majira ya saa kenda , saa za hapa nyumbani.

Gari moja ambayo ikitembea kwa mwendo wa kasi iligonga mwendesha pikipiki moja pamoja na mteja wake. Mwendesha pikipiki huyo alijeruhiwa vikali, ila mteja alipatwa na majeraha kidogo.

Mwendesha pikipiki alipelekwa hima kwenyi hospitali Biopharm ili apewe matibabu.

Duru zetu zaeleza kwamba dreva wa gari alikuwa ametumia mvinyo mno, kwani kwenyi nafasi yake ya kukaa, kuligunduliwa chupa munane za pombe aina sapilo.

Gari iliweza kuokolewa na askari polisi mikononi mwa waendesha pikipiki wengine, ambao walitaka kuichoma kwa moto. Dreva alibaki mikononi mwa askari polisi akilala, duru zetu zafahamisha.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire