Kivu ya kaskazini : Hali yanaendelea kukwama huko Kasindi wilayani Beni hii asubui ya juma pili, kuendelea kupinga vikosi vya MONUSCO

Hali imekwama mara tena kweyi mpaka wa Kasindi. Ni katika lengo la kuendelea kupinga vikosi vya MONUSCO humu nchini, hususan mjini Béni na jimboni Kivu ya kaskazini kwa jumla. Waandamanaji wenyi hasira wakitembea barabarani wakibeba jeneza yenyi chapa MONUSCO.

Upande wa senta ya Kasindi, kazi zimezorota kijamii na kiuchumi. Wafanya byashara kwenyi barabara Kasindi Béni, hawaondoke ama kuingiza bidhaa toka nje. Nafasi ya kazi ni wazi, ijapo walinzi wa usalama peke.

Kutokana na duru zetu, vijana waandamanaji wamepinga kurudi kwa wafanya kazi wa MONUSCO kupitia mpaka huo wa Kasindi unaounganisha nchi ya DRC na Uganda. Vijana wakibeba jeneza yenyi kuandikwa:  » Umoja wa kimataifa ni mwili usio na uhai unaotembea . »na kadhalika.

Duru zetu huongeza kwamba kamati ya usalama ya mahali yafanya uchunguzi wa waandamanaji, ili wasianguke ndani ya vitendo vya ujeuri, muda wote wa maandamano.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire