Wanamemba wa Lucha wamewekwa kizuizini hii juma tatu tarehe 1 Agosti ,kwa ruhusa yake mea wa mji wa Kisangani Bwana Louis Alasso.
Huyu alikataza maandamano yoyote île yenyi kupinga Monusco , ambaye kwa sasa ni vuta ni kuvute na wakongomani. Zaidi ya miaka ishirini ya MONUSCO bila kutekeleza amani.
Vijana wengi wa Lucha walikusanyika tangu juma pili alfadjiri kwenyi nafasi Place des Martyrs, ambako walianza maandamano ya amani dhidi ya MONUSCO, wakisema hakuna mafaa kwa shirika hili la kimataifa kubaki kwenyi ardhi ya DRC. Barabarani, wakiimba nyimbo zenyi kupinga shirika hili.
Dakika chache baada ya kuondoka, walijikuta kusambazwa kinyama na askari polisi. Wengi miongoni mwao, waliwekwa kizuizini kwenyi ofisi ya polisi ya mji.
Duru zetu toka Kisangani zanena kwamba, ma saa ishirini na nne mbele ya maandamano, mea wa mji Louis Alasso alikataza maandamano yoyote île kuhusu MONUSCO. Na ndio ilipelekea kuwaweka kuzuini kwenyi kituo cha polisi wanamemba hawo wa Lucha.
Watetezi kadhaa wa haki za binaadam waomba vijana hawo waachiliwe huru, wakilaumu vitendo vya kinyama vya askari polisi dhidi ya wanainchi hao.
Tukumbushe kwamba ni tangu kasoro iliyojitokeza kwenyi mpaka wa Kasindi. Vikosi vya MONUSCO kufyatuwa risasi kwa raia na kusababisha vifo na majeraha, ndio chanzo cha maandamano hayo mjini Kisangani.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.