Habari toka mjini Bukavu zaeleza kuonekana kwa mwili usio na uhai wa mwanaume kando na idara ya madini upande wa ofisi ya bunge la jimbo mtaani Ibanda saa za alfadjiri.
David Cikuru aliyetowa habari kwenyi vyombo vya habari aeleza kwamba, ni visa aina hiyo vyaripotiwa kila mara mtaani humo. Akiongeza kwamba asilimia sitini vya visa hivyo, ni watu kufariki wakitumia mvinyo kiasi, yaani pombe za kulevya.
Prezidenti huyo wa shirika la raia mtaani Ibanda aeleza kwamba miili isio n’a uhai yaripotiwa hasa kwenyi mto Ruzizi, kwenyi ziwa Kivu na hâta pembezoni mwa mtaa wa Ibanda.
David Cikuru alaumu utumiaji wa pombe hizo za kulevya kwa kuwa ni zenyi kuleta hasara kubwa.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.