Kivu ya kaskazini : Kumbukumbu ya maelfu ya wakongomani waliopoteza maisha ndani ya vita vya uporaji wa mali ya nchi

Mwanzilishi wa maoni Kujitegemea Dady Saleh.

Mchambuzi kisiasa pia mwanzilishi wa ideolojia Tujitegemee Dady Saleh ,anena kukerwa moyoni, kwa kuwa raia waendelea kutowa hesabu zisizo kamili kuhusu walio poteza maisha yao tangu mwanzoni mwa vita mbali mbali hadi sasa raia wakipinga kata kata MONUSCO kubaki nchini DRC. Kwa kuwa hakufaulu kutekeleza amani nchini.

Alinena hayo hii juma nne tarehe 3 julai 2022 mjini Goma. Siku iliyo chukuliwa na raia kwa jumla, ili kukumbuka wakongomani wote walio aga dunia katika vita vilivyo rahisisha uporaji wa mali ya DRC.

Dady Saleh aongeza kwamba ingelikuwa heri serkali kukabizi idadi ya wahanga siku bila kazi, kwenyi nchi nzima na hâta kwenyi ngazi za kimataifa.

Baada ya serkali kukubali siku hiyo pamoja na utafwiti kwa kukusanya habari mhimu, ifwatayo ni kuomba sheria itekelezwe dhidi ya wahanga.

« Inabidi jambo hili lizungumzwe, kwani ni mauaji ya kimbari ndio ilifanyika. Maana kulionekana vifo vya watu wengi kiholela. Watu wakiuliwa kwa risasi, hâta kwa mikono . Ni kusema ni mauaji ya alaiki ndio inaendelea. Ndio maana siku hiyo ikubaliwe kiserkali, na hali hiyo ikome. Na kila mtu atafahamu kwamba anapofanya mauaji, wakongomani wote watainuka hâta kwenyi ngazi za kimataifa. Inabidi kukusanya tarehe kadhaa zinazo patikana ndani ya ripoti mbali mbali, kwa kupata mwangaza kuhusu mauaji iliyo fanyika, » aeleza Dady Saleh.

Ilikuwa fursa kwa wahanga wa mauaji ya kimbari yanayo lenga uchumi, kuondowa woga, wakitowa habari mhimu zitakazo saidia kwa kuandika historia kamili.

Mchambuzi kisiasa Dady Saleh afahamisha kwamba uchunguzi utafanyika namna tatu; kihistoria, kiutu na katika uhuru.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire