Kivu ya kaskazini : Mapigano imeanza mara tena kati ya waasi ya M23 na jeshi la taifa

Mapigano imeanza mara tena wilayani Rutshuru kati ya waasi wa M23 na jeshi la taïfa FARDC baada ya karibu mwezi moja wa ukimya. Ni kwenyi eneo la Kisigari vijiji vya Kanomnbe na Nyamisisi.

Aimé Mukanda moja wa waheshimiwa wa Rutshuru akihojiwa na vyombo vya habari alaumu uporaji wa mali ya raia unaofanyika na waasi wa M23. Pamoja na hayo ashukuru juhudi za askari jeshi FARDC, ambao walitowa Kijiji moja mikononi mwa waasi.

Aimé Mukanda aomba askari jeshi kufukuza waasi maeneo wanayo vamia , kwani hapa karibuni tayari wataweza kuzibiti eneo la Rumangabo.

Tukumbushe kwamba baada ya vikosi vya MONUSCO kushutumiwa katika mauaji pa Kasindi Beni, waasi wa M23 wameanza mara tena mapigano wilayani Rutshuru.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire