Bwana Gérard TADEBOIS anena hayo hii juma tano tarehe 3 agosti baada ya kukutana na liwali wa jimbo Théo Ngwabidje Kasi. Miezi tatu tangu kuanzishwa kwa kazi yaani mwezi mei, watu 1300 wamekwisha kupata kazi kupitia kiwanda. Kazi zinahusu kupanda na kuvuna mimea
kwenyi eneo lenyi hekta 1000, na kutowa tani 3000 n’a 4000 za sukari. Ni katika lengo la kutaka kazi za kiwanda zianze, gari na shamba.
Duru toka chumba cha upashaji habari kwenyi ikulu ya liwali chanena kwamba , kiwanda cha sukari cha Kiliba, kinatarajiya kutowa tani 25 za sukari kwa mwaka, na kuwapa kazi watu 3000 mwaka ujao.
Hiyo ni katika lengo la kurudisha sura la kiwanda hicho, ili wafanya kazi, raia na eneo nzima warudie hali yao ya maisha kupitia kiwanda hicho cha sukari.
Liwali wa jimbo aliomba wahusika na kiwanda kuboresha kazi, kutowa matunda bora, na hata kupanga beyi nzuri ili raia watumie bila shida matunda ya kazi. Akiongeza kwamba hiyo itapelekea maendeleo kiuchumi na kijamii ya jimbo, ya mji wa Uvira na hata eneo nzima. Na hiyo ni matakwa yake Raisi wa DRC.
Kiongozi wa kiwanda cha sukari alisema kwamba kazi zitaanza kinaga naga tarehe 1 septemba 2022.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.