Kivu ya kaskazini : Goma Fleva média on line itatangaza kipindi cha tatu ; watu waliofaulu ndani ya kazi wakichukuwa nafasi ya kwanza ndani ya sekta zao, watapewa tuzo

Kunaandaliwa hii ijumaa tarehe 5 Agosti 2022, sherehe ya kutangaza rasmi watu kadhaa waliofaulu ndani ya kazi zao, wakichukuwa nafasi ya kwanza katika sekta zao, watatolewa tuzo.

Hayo yalifahamishwa wakati wa mkutano na wandishi habari hii alhamisi tarehe 4 Agosti 2022 mjini Goma naye Dany Izinga kiongozi wa Goma Fleva.

Sherehe zitafanyika kwenyi chumba cha mapokezi Serena tukiwa jimboni Kivu ya kaskazini.

« Kesho tuta timiza kipindi cha tatu kuhusu kazi tuliweza kuandaa. tangu mwaka 2019. Kila mara tunachaguwa watu mia moja ambao ni viongozi wenyi kutumika kuhusu maendeleo ya mjini wa Goma. Ni watoto wa Goma ambao wametumika sana ndani ya sekta mbali mbali. Mfano mziki, userumala, ujenzi, utetezi wa haki ya binaadam, kiganga, usanii, wandishi habari na kadhalika. Watu watakao pewa tuzo na wasindikizi wao, ndio watafika kwenyi sherehe, » anena Dany Izinga.

Kiongozi wa Goma Fleva anena kwamba sherehe hiyo ya ijumaa itatangazwa kwenyi mtandao wa kijamii Facebook. Na kwamba juma mosi, ni wakati wa kutangaza majina ya watu wote kwenyi orotha, wakipewa vitambulisho.

Huyu aongeza kwamba mbele ya kutangaza matokeo, média yake inakuwa ikiandaa kampeni. Huku wakiomba raia kuonyesha mtu ambaye ametumika kazi zake vizuri, akichukuwa nafasi ya kwanza hasa. « Baada ya raia kutaja mutu huyo, uchunguzi unafanyika ili kujuwa kama mtu aliyetajwa kweli ametumika vizuri na anastahili. Na hapo anawekwa kwenyi orotha, » afasiria Dany Izinga kiongozi wa Goma Fleva.

Akihojiwa kuhusu viongozi kila mwaka watajwa wenyewe kuchukuwa nafasi ya kwanza, Bwana Dany anena kwamba,watu wakitumika vilivyo, sherti wachukuwe tu nafasi ya kwanza, pasipo upendeleo.

Mwishowe aliomba raia kufanya kazi vizuri ili siku moja wapate kutajwa kwenyi mstari wa mbele miongoni mwa watu wenyi kufanya kazi vizuri.

« Kazi hizo zinasapotiwa na mashirika kadhaa za hapa nyumbani, yaani Kin marché, shirika zingine husika na majengo na kadhalika« , anena Dany Izinga akizungukwa na wasaidizi wake.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire