Kivu ya kaskazini/Walikale: watu munane wamekwisha fariki dunia kutokana na ugonjwa wa kuhara

Wilaya ya Walikale.

Visa munane vya watu wenyi kufariki na ugonjwa wa kuhara viliripotiwa eneo la Toto, wilayani Walikale jimboni Kivu ya kaskazini.

Mwanabunge Prince Kihangi mchaguliwa wa Walikale aomba liwali wa jimbo pamoja na idara ya afya jimboni, kuchukua hatua, ili kukomesha ugonjwa huo, unaotokana na mikono michafu.

Katika tangazo lake, Mwanabunge Prince Kihangi anena kwamba visa vingi vya wagonjwa vinahudumiwa na vituo vya afya vya mahali. Na kwamba vituo hivyo vina shida ya dawa.

Ndio maana mchaguliwa huyo aomba liwali wa jimbo kufanya yote iwezekanayo, ili kukomesha ugonjwa huo. Na kwenyi idara ya afya, kutuma timu la kwanza litakalo tolea tiba ya kwanza kwa wagonjwa. Na kwa wanamemba wa kamati la maendeleo la mahali, kuheshimu kanuni za usafi, ili kuepuka kuambukiza ugonjwa yenyewe.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire