Goma : Miili kumi isio na uhai miongoni mwa kumi na tatu wahanga wa maandamano kwa kupinga Monusco, inapelekwa kwenyi shamba la wafu Makao wilayani Nyiragongo

Mbele ya kujielekeza kwenyi shamba la wafu, jeneza kumi zililazwa mbele ya uwanja wa kandanda » stade de l’unité » pa Goma jimboni Kivu ya kaskazini.

Jamaa, ndugu na marafiki wa wahanga wanaimba nyimbo, wakionyesha hasira dhidi ya MONUSCO.

« Kwenyi mabango zao;  » Hatutaki tena MONUSCO, anauwa wakongomani, uongozi wa kijeshi iondoke, Rwanda inafanya mauaji nchini DRC, tutaacha maandamano hadi MONUSCO atakapo ondoka kwenyi ardhi ya DRC, » watowa machozi waandamanaji, wakilia ndugu zao.

Nafasi kote mjini hakuna kazi, waandamanaji wakivaa vazi nyeusi, na vitambaa kichwani. Umati kwenyi uwanja wa kandanda na kote barabarani, kupita mahali hapo ni vigumu.

Kwa sasa umati unasindika miili katika hali ya nyimbo za huzuni, kwa kupiga filimbi.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire