Goma: Miili kumi ya wakongomani waliofariki katika maandamano ya kupinga Monusco imepelekwa kwenyi makao ya mwisho

Raia wakisindikiza miili.

Kilio na machozi, huzuni, heshima, ilionekana kwa wakongomani walio wengi, wakisindikiza miili za ndugu zao, hadi kwenyi makao ya mwisho. Wakati huo, kazi zilifungwa popote pale, ofisini kama barabarani. Waandamanaji wakivaa vazi nyeusi na kufunga vitambaa kichwani. Wakilazimisha Monusco aache uvamizi wa ardhi ya DRC, arudi kwao, na kuwa hakufaulu kwa kazi, anauwa wakongomani.

Njiani kwenda kwenyi shamba la wafu kulitokea kasoro. Hali ya vuta nikuvute ilionekana kwenyi kituo cha Monusco kwenyi uwanja wa ndege. Hali iliyosababisha mara tena majeraha.

Mwanabunge wa taïfa Jean Baptiste Kasekwa.

Mwanabunge Jean Baptiste Kasekwa alishiriki kwenyi sherehe za mazishi. Kutokana na hali iliyoko nchini, mchaguliwa huyu jimboni Kivu ya kaskazini, aliomba aondoshwe kazini waziri wa taïfa husika na mambo ya nje. Aliahidi afikapo bungeni, kuomba wenzake waandike kibarua ili afukuzwe madarakani waziri husika na mambo ya nje nchini DRC.

Tufahamishe kwamba waandamanaji walisema kutoacha maandamano, kabla Monusco anaendelea kuvamia Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire