Bukavu : Liwali wa jimbo la Kivu ya kusini aendelea na kazi za ujenzi mtaani Bagira

Duru toka ikulu ya liwali zanena kwamba kazi hizo zasapotiwa kwa asilimia tisini na serkali ya jimbo. Zikirahisisha mawasiliano kwa mitaa tatu ya mji wa Bukavu.

Pamoja na hayo, serkali jimboni kupitia Liwali wa jimbo Théo Ngwabidje, inajihusisha na kazi za kutengeneza na kukarabati barabara ndani ya mtaa wa Bagira, ambayo pia ni matakwa yake Raisi wa DRC.

Mfereji kubwa Pharmakina unajengwa, ikiwa na urefu wa mita 85, nafasi ya kupeleka maji yenyi urefu wa mita 150, ikipelekea maji ya kata Mulambula hadi mto Chula. Pia mingazi inatoka kwenyi shirika Pharmakina hadi senta Kanjira ya mita 270 ya urefu na mita 25 upana.

Alipotembelea huko, Liwali wa jimbo Théo Ngwabidje aliahidi kuzidisha miradi aina hiyo, kwa manufaa ya raia.

Upande wao, raia walionyesha hitaji ya barabara Kalengera Kahero, kuelekea ulalo Mugabo ambao ulijengwa sasa. Liwali aliahidi kutembelea nafasi hiyo pamoja na timu lake la kiufundi, ili kuchunguza la kufanya.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire