
Watenda maovu ishirini na tatu miongoni mwao moja munyarwanda, walionyeshwa hazarani, mbele ya waziri makamu wa kwanza Daniel Aselo, mjini Kinshasa. Walionyeshwa na askari polisi, wakishutumiwa shambulizi, wizi kwa kumiliki silaha kati ya mji wa Kinshasa na Kongo central. Ilikuwa mbele ya jumba la serkali, mtaani Lingwala.
Duru za mahali zaongeza kwamba wevi hawo wapatikana ndani ya kundi tatu; wakiwa na silaha za vita, risasi, tumbako aina bangi na silaha zingine za asili. Hawa watembea kila mara ndani ya gari na kwenyi pikipiki. Wakiendesha vitendo vya wizi, mauaji, unyanyasi, byashara ya tumbako kunako nafasi kadhaa nchini DRC.
Wakati huo, vikosi vya polisi, vilifahamisha kwamba miongoni mwa watenda maovu mulikuwemo , mtoto wa mpiga picha moja wa redio ya taïfa Rtnc. Mtoto huyo aliuwawa nyumbani kwake tarehe 22 julai. Ni katika mtaa wa Kimbaseke mjini Kinshasa.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.