Bukavu/ Panzi: Norbert Basengezi Katintima ajitowa katika ujenzi wa uwanja wa kandanda Parade

Akizungumza na raia kupitia viongozi wa tabaka za chini, Liwali wa zamani wa jimboni Kivu ya kusini Norbert Basengezi Katintima aahidi kujihusisha katika ujenzi wa uwanja wa kandanda katani Panzi. Uwanja unaoitwa Parade.

Norbert Basengezi alisema kwamba ujenzi wa uwanja huwo ni miongoni mwa miradi ya ujenzi wa mji wa Bukavu. Akinena shirika la kimataifa la kandanda FIFA liliweza aahidi ujenzi wa uwanja huwo,

Huyu alisema kwamba atakutana n’a Liwali wa jimbo, ili kuzungumzia swala hilo. Akionyesha mafaa ya ujenzi wa uwanja huwo, kwa kuwa kata Panzi itageuka mtaa hapa karibuni. Pamoja n’a hayo, barabara zitajengwa hapa na pale ndani ya kata hiyo, zitazo pelekea kwenyi uwanja wa kandanda wa Panzi.

Jambo hili lilimu furahisha Redouta Mweresi ambaye ni kiongozi wa shirika la raia katani Panzi. Alishukuru kitendo hicho toka liwali wa zamani jimboni Kivu ya kusini.

Tukumbushe kwamba tangu Siku nyingi uwanja huwo, ulikuwa ukishambuliwa na watu wenyi nia. Ujenzi wa uwanja huwo ni jibu kwa kukomesha shambulizi hilo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire