Goma: Mwanabunge wa taïfa Josué Mufula aendelea na kazi za utetezi bungeni

Akiwasili mjini Goma hii juma tatu tarehe 15 Agosti 2022, Mwanabunge wa taïfa Josué Mufula anena kuja likizoni baada ya matunzo nje ya DRC. Akitowa mbele ya yote pole kwa jamaa zote zilizo kumbwa na misiba. Hayo ni kutokana na hali ya heka heka kati ya raia na MONUSCO, iliyopelekea vifo, majeraha na maafa mengine mengi. Akijibu kwa maswala ya wandishi baadae

Akihojiwa kuhusu kazi alizozifanya bungeni kwa kutetea raia, mchaguliwa wa Goma, Josué Mufula anena kwamba alipigana ili kukomesha ushuru RAM, kuendelea kutetea wahanga wa mripuko wa volkeno ,na akina mama wa soko kwa jina Kisoko wapewa mikopo na waendesha kazi zao kama kawaida.

« Sisi tumefanya kazi mhimu bungeni, tumepiganisha kwa nguvu ushuru RAM na imekwisha kukoma. Tunaendelea kutetea wahanga wa mripuko wa volkeno. Pamoja na hayo, akina mama wa soko Kisoko wamepewa mikopo midogo midogo. Ukifika hapo utakuta akina mama wakiendesha kazi zao bila shaka. Tutakapo rudi bungeni katika kikao kinacho husu bajeti, nitagusia swala kuhusu kuboresha maisha ya askari jeshi na askari polisi. Kwa maana jeshi ndiyo nguvu za nchi
Nitaendesha utetezi kwa maswala zingine nyingi huko bungeni, aongeza Josué Mufula Mwanabunge wa taïfa.

Kuhusu kuvamiwa kwa Bunagana na waasi wa M23 muda wa miezi mbili na zaidi, Josué Mufula anena kwamba amekwisha kuzungumzia bungeni swala ili kuboresha maisha ya askari jeshi. Na kwamba inabidi hali ya maisha ya jeshi iboreke, ili afanye kazi vilivyo. Na kuhusu kuingizwa kwa vikosi vya Burundi kwenyi ardhi ya DRC ili kutumika pamoja na FARDC, Mwanabunge Josué Mufula anena kwamba atafwatilia swala hilo afikapo bungeni.

Juvénal Murhula.


Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire