Raisi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo amepewa uongozi wa muungano wa nchi za Afrika SADC, wakati wa kilele cha 42 mjini Kinshasa nchini DRC.
Aliyemkabizi madaraka ni Raisi wa Malawi Daktari Lazarus Chakwera, mbele ya maraisi wengi wa Afrika, walioshiriki kwenyi mkutano huo mkuu.
Kiongozi mpya wa SADC Félix Antoine Tshisekedi alichukuwa hatua ya kukubali kutumika ajili ya umoja ma inchi. Pamoja na hayo, kuinua viwanda katika sekta ya kilimo na ya madini, ili kuwe na uchumi wa pamoj na wa kudumu.
Félix Antoine Tshisekedi akionyesha umuhimu wa kuinua majengo kwenyi muungano SADC , ambayo amekabizwa madaraka.
Pamoja na hayo, alishukuru nchi za Afrika ya kusini, Tanzania na Malawi zilizotowa vikosi vyao ndani ya MONUSCO ajili ya kutekeleza usalama mashariki mwa DRC, ijapo nchi ya Rwanda yaendesha shambulizi dhidi ya nchi hiyo.
Kilele hicho kina mada; kuinua viwanda katika sekta ya kilimo na ya madini, ili ya uchumi wa pamoja na wa kudumu,
Walikuweko viongozi wengi wa Afrika, ili ya kuleta mcango yao katika kazi kubwa kama na hiyo, ajili ya ujenzi wa bara la Afrika.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.