Goma: Liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini arudi mjini Goma kutoka Beni na Butembo, ambako alipongeza raia kutokana na hali mbovu iliyojitokeza huko

Akiwasili kwenyi uwanja wa ndege kutoka mjini Béni na Butembo, Liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini Constant Ndima Kogba anena kurudi ziarani. Alijielekeza huko katika lengo la kujioneya hali iliyoko, kutokana na raia wanaopinga kubaki kwa Monusco nchini DRC.

« Kutokana na hali hiyo, Raisi wa DRC kupitia waziri mkuu alituma ujumbe wa mawaziri mjini Béni, ambako walipeleka ujumbe wake na kutowa pôle kwa wahanga wa machafuko ilijitokeza kwa kupinga Monusco, » anena liwali wa jimbo.

Akigusia pia shambulizi la wanamugambo ADF, dhidi ya jela kuu la Kakwangura pa Butembo, ambalo lilipelekea pia vifo. Akiongeza kwamba ni katika lengo hizo ndipo alijielekeza huko ili kujioneya kipi kifanyike, kwa ngambo ya serkali ya jimbo.

Kuhusu shirika la raia, ambalo limepanga kuendesha maandamano tangu wilaya hiyo hadi mjini Goma, kutokana na usalama mdogo eneo hilo, liwali anena kuwa mbele aondoke mjini Goma, alikutana na shirika la raia na miungano memba.

« Mimi nilikutana na shirika la raia pamoja na miungano memba. Wakiniambia kwamba hakuna kinacho fanyika kuhusu usalama. Niliwaambia wabaki kimya. Askari jeshi wanafanya kazi. Nazani mumesikia kazi zenyi kufanyika na jeshi kwenyi mapambano. Serkali inajihusisha Pia na diplomasia, na yote inaambatana, » aeleza liwali wa jimbo Constant Ndima Kogba.

Juvénal Murhula.


Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire