Kivu ya kaskazini/ Butembo : Mea wa mji atangaza kuondoka kwa vikosi vya MONUSCO eneo hilo

Katika tangazo lake la juma mosi tarehe 20 Agosti 2022, mea wa mji wa Butembo, kamisa mkuu Mowa Baeki Roger ahakikisha kuhamishwa kwa vikosi vya MONUSCO mjini Butembo, jimboni Kivu ya kaskazini.

Kwa kutekeleza mpango huo, mea wa mji aomba raia ku uheshimu, ambao ulipangwa na viongozi wa serkali pamoja na MONUSCO.

Tangazo hilo lapanga tarehe ya kuondoka na mahali pa kujielekeza.

 » Tangu tarehe 20 hadi 21 Agosti, tangu saa mbili hadi saa tano usiku, gari zitatoka Beni hadi Butembo, ili kuchukua vifaa. Usiku wa tarehe 21 hadi 22 Agosti, tangu saa tatu hadi saa saba usiku, gari zitatoka Butembo hadi Lubero, kuhusu tu kazi hiyo. Mcana wa tarehe 22Agosti, tangu saa tatu hadi saa tano, kuondoka kwa vikosi URUBATT , tangu Lubero hadi Goma, kupitia helikopta. Usiku wa tarehe 22 hadi 23 Agosti, saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubui, kuondoka kwa gari kumi na tano, tangu Lubero hadi Rwindi. Usiku wa tarehe 23 hadi 24 Agosti, tangu saa tatu hadi saa saba usiku, kuondoka kwa gari Rwindi hadi Kiwanja« , tangazo la mea wa mji wa Butembo lafahamisha.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire