Kivu ya kusini : Jengo kubwa lenyi gorofa tano laanguka, na kusababisha vifo na majeraha mjini Bukavu

Nyumba yenyi gorofa tano iliyokuwa ikijengwa imeanguka hii juma mosi kuamkia juma pili tarehe 21 Agosti 2022. Watu kufunikwa na wengine kujeruhiwa.

Duru mjini Bukavu zaeleza kwamba ajali ilifanyika kwenyi eneo la Résidence, mbele ya jumba la mapokezi le Cadre, kunako barabara kuelekea kwenyi makao ya liwali wa jimbo.

Duru zaongeza kwamba miongoni mwa watu waliopatikana nafasi hiyo, 11 tayari wamepotea na 7 wamejeruhiwa na kupelekwa hima hospitalini.

Hali iliyopelekea waziri husika na mji pia mkaji jimboni Kivu ya kusini, kujielekeza mahali hapo pa ajali. Chanzo ni kwamba, nyumba hiyo ilikuwa ikijengwa na vifaa vinavyozaniwa kuwa vibovu.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire