Kivu ya kaskazini/ Béni: Raia 17 wauliwa munamo Siku tatu

Watu 17 wamepoteza maisha kutokana na shambulizi la wanamugambo ADF, katika vijiji vya MUTEU SIRO na BEU MANYAMA wilayani jimboni Kivu ya kaskazini. Mauaji hayo yafanyika munamo siku tatu.

Duru kutoka Beni zaeleza kwamba, raïa tano waliuliwa tarehe 29 Agosti na kumi na mbili wakiuliwa tarehe 30 Agosti 2022, ambayo inaongeza hesabu.

Ijapo raia kukimbia maskani yao, hawa wajikuta kushambuliwa na wanamugambo ADF, mahali wanakimbilia. Jambo ambalo lahatarisha kila leo maisha yao.

Tufahamishe kwamba ni tangu miaka chungu télé raia wa Béni ni wahanga wa mauaji, ikisababishwa na waasi ADF. Ijapo malalamiko ya miungano ya shirika la raia pamoja na wabunge wazali wa huko, hali yaendelea kukwama.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire