Kivu ya kaskazini : Bwana Jean Bosco Kaboy Bwivu atowa pole kwa raia jimboni humo kuhusu maafa ya vita, inayosababishwa na magaidi wa M23

Prezidenti wa chama cha kisiasa ADES Jean Bosco Kaboy Bwivu apatikana ziarani jimboni Kivu ya kaskazini na kusini, tangu majuzi akitoka mjini Kinshasa.

Alifahamisha kwamba anakuja kujioneya hali ya afya ya chama chake, jimboni Kivu ya kaskazini na kusini.

Kuhusu hali ya usalama mashariki mwa DRC, huyu asema kuunga mkono serkali ya DRC kwa kupiganisha usalama mdogo. Pia atowa pole kwa raia wote jimboni Kivu ya kaskazini, wenyi kupoteza maisha kila leo. Hali inayosababishwa na waasi wa M23.

Prezidenti wa chama ADES Jean Bosco Bwivu anena kuwa chama chake cha kisiasa ni tayari kushiriki kwenyi uchaguzi mwaka 2023. Na hii ni moja wapo wa lengo ya ziara yake Kivu ya kaskazini na kusini.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire