Goma: Ndege ya aina Helikopta ya shirika la mpango wa chakula ulimwenguni PAM imeanguka karibu na mji wa Goma

Ndege aina Helikopta ya shirika la mpango wa chakula ulimwenguni PAM imeanguka hii ijumaa tarehe 2 septemba 2022, eneo la Rusayo, karibu na mji wa Goma, wilayani Nyiragongo, Kivu ya kaskazini.

Kiongozi wa Rusayo Janvier Bangumya anena kwamba hakuna mtu aliyefariki dunia kutokana na ajali hiyo. Akiongeza kwamba waliojeruhiwa walipelekwa kwenyi vituo vya afya ili watolewe matibabu.

« Ndege ilianguka karibu na shamba la kuhifadhi wanyama la virunga. Hakuna mtu aliyepoteza maisha ndani ya ajali. Waliojeruhiwa walipelekwa na raia hima kwenyi hospitali ili wapewe matibabu », aeleza kiongozi huyo.

Mnenaji kwa muda wa MONUSCO Ndege Khady aliyetajwa na wenzetu wa Agoragrands lacs, anena kwamba ajali hiyo ilitokana na hali ya kiufundi.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire