Kivu ya kusini/Kabare : Mtu anayezaniwa mwizi aliuliwa na raia kwa kujilipishia kisasi

Mtu mwenyi kushutumiwa wizi aliuliwa kwenyi kijiji Kabushwa pa Irhambi Katana, wilayani Kabare jimboni Kivu ya kusini.

Duru za mahali zaeleza kwamba mtu huyo alikutwa ndani ya wizi majira ya saa kumi na mbili. Wakaazi kumpiga kama nyoka hadi kifo.

Shauri la vijana pa Irhambi Katana lalaumu kitendo hicho na kuomba raia kuarifu kila mara vyombo vya sheria.

« Ni majira ya saa kumi na mbili, kijana Dieumerci alikutwa akiiba. Ndipo raia kumpiga kama nyoka, hadi kuaga dunia. Tunalaumu kitendo hicho, na kuomba raia kutoendelea. Kwa kuwa hali hiyo yapelekea vifo hâta kwa watu wasio na hatia. Pamoja na hayo, serkali hushindwa kufanya uchunguzi, » duru zaongeza.

Tufahamishe kwamba eneo hilo lashambuliwa kila leo na watu wenyi kumiliki silaha, na wasiojulikana. Kiongozi wa shauri la vijana pa Irhambi Katana aunga raia mkono kwa kupiganisha usalama mdogo makwao, ila awaomba kuharifu kila mara vyombo vya usalama.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire