Kivu ya kaskazini/ Rutshuru : Mishahara ya walimu yapokonywa

Habari toka mtetezi wa haki za binaadam wilayani Aimé Mukanda zaeleza kwamba tangu mwaka 2021, milioni 50 franka za Kongo mishahara ya walimu imepokonywa. Pesa ambazo zilipangwa kulipa walimu 108 wa Vitshumbi na 80 wa Kibirizi eneo la Bwito wilayani Rutshuru.

Kutokana na ujumbe wake Aimé Mukanda, wanaozaniwa kuiba pesa hizo, ni kiongozi moja wa shule la msinji la Vitshumbi. Huyu alinaswa na kutupwa ndani ya jela kuu Munzenze.

Upande wa shule la Kibirizi, kiongozi wa shule la msinji Kishishe/ Bwito, aliyeshutumiwa tayari amenyatuka na zaidi ya milioni 23 franka za Kongo, mahali pasipo julikana. Duru zetu zaongeza kwamba, kiongozi huyu aliungwa mkono ndani ya wizi na Padri moja wa parokia ya Katwe. Huyu pia ametupwa korokoni.

Mtetezi wa haki ya binaadam wilayani Rutshuru Aimé Mukanda aomba shirika Caritas kufanya yote iwezekanayo ili kufikisha mishahara ya walimu vijijini, ama kutuma pesa za walimu kwa njia ya mtandao.

Na kama sivyo, Aimé Mukanda aomba shirika Caritas, kuacha nafasi kwa shirika lingine litakalo rahisisha kazi hiyo.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire