Kivu ya kaskazini/ Goma : Baada ya wizara ya elimu ya shule la msinji, sekondari pia ufundi kutangaza kuanzishwa kwa shule hii tarehe 5 septemba, raia walio wengi waonekana kukosa msimamo

Ni hii tarehe 5 septemba 2022, ndio wizara ya elimu ya msinji, sekondari na kiufundi imetangaza kuanzishwa kwa shule nchini kote Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Mjini Goma kwa peke na jimboni Kivu ya kaskazini kwa jumla, raia walio wengi wajiswali kuhusu hali ambamo shule zitaanzishwa. Wadadisi wa mambo hawajuwi namna gani kazi za shule zitaanza, hasa kwenyi eneo zenyi kukumbwa na vita. Mfano wa vijiji kadhaa vya Rutshuru, ambavyo ni shamba kwa leo la waasi wa M23. Bila kusahau wilaya ya Beni, ambako wanamugambo ADF waendelea na vitendo vya ukatili.

Upande wa wazazi, wengi waeleza kwamba hawana pato kwa kununua vifaa vya shule, yaani uniform, buku na kadhalika. Wachuuzi wa vifaa vya shule watandika byashara kila leo, pasipo kupata wateja. Kwenyi barabara na soko, mteja aonekana moja kwa moja, akinunuwa kwa uzembe, kulingana na pato yake ndogo.

Pamoja na hayo, kushindwa kiasi kwenyi mtihani wa serkali, kwa wanafunzi wa shule la sekondari jimboni Kivu ya kaskazini, ni moja wapo ya wazazi wenyi pato ndogo, kukosa bidii na hata matumaini.

Tufahamishe kwamba tangu kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa serkali nchini DRC, na kulingana na kushindwa kwa wanafunzi wengi jimboni Kivu ya kaskazini, wazazi wengi pamoja na watoto wao, wasema kushitushwa moyo kulingana na matokeo isiyo furahisha.

Baada ya matangazo, shule nyingi zilionekana kutofaulu kote jimboni Kivu ya kaskazini. Na katika shule zingine, ni idadi ndogo ya wanafunzi ilionekana kufaulu.

Nazo shirika za kutetea haki ya walimu mjini Kinshasa, hazina kauli moja kuhusu kufungulia kwa shule hii juma tatu tarehe 5 septemba 2023. Ni mfano wa shirika la kutetea haki za walimu wa shule za kikatoliki SYNECATH, ambalo laomba walimu kwenda shuleni wakingojea moja kwa moja jibu la serkali kuhusu madai yao. Shirika likisema kwamba mambo yanaendelea kufaulu upande wa serkali kwa kuboresha kazi za walimu; mfano wa watoto kusoma bure, na juhudi kwa kuongeza mishahara ya walimu na kadhalika.

Ijapo mashirika zingine zapinga kurudi kwa kuwa serkali hakujibu kwa madai yao. Mfano ya makubaliano ya Mbwela kuhusu kuwapa walimu mishahara kiwango cha dola 400 za marekani, kulipa sawa sawa walimu mishahara yao, kulipa walimu wapya, na hata wa zamani wasiopata mishahara na kadhalika.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire