Akitokea mjini Kinshasa hii alhamisi tarehe 8 septemba 2022, liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini Constant Ndima Kogba amezungumza na wasafiri, wahanga wa kuvurugwa kwa mipango ya safari ya ndege ya shirika CAA. Na hata mashirika mengine, zenyi kutumika kwa njia ya anga nchini DRC.
Wasafiri hawa walifanya kikao kwenyi uwanja wa ndege wakisubiri kuja kwake liwali. Wakisema kuchoka na kuarishwa kwa safari za ndege CAA kila leo. Hii ni namna ya kuvunja mipango yao ya safari, na hata ya kazi.
Wakati huo, liwali alijaribu kuwapatanisha na shirika la ucukuzi kwa njia ya anga CAA, ili waweze kusubiri.
« Natoka mjini Kinshasa. Hali ni moja kote nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Mjini Kinshasa, hata gari nyingi, na pikipiki na vinginevyo havitembee. Ni kutokana na ukosefu wa mafuta ya petroli. Juma pili, nilifanya safari mjini Kinshasa. Ndege iliyonichukuwa iliaribika na kwa sasa haitembee. Shirika CAA linakumbwa na shida, kwa kuwa linatumia ndege mbili kubwa kwa safari, ila moja peke ndio yatembea. Kuna shida ya kusafiri kwa sasa kote nchini DRC. Natoka kuzungumza na viongozi wa shirika la uchukuzi angani RVA mjini Goma, wameahidi kwamba suluhu litapatikana tangu juma tatu ijayo, » afasiria liwali wa jimbo mbele ya wateja wa CAA.
Constant Ndima awalika mara tena kuwa na subira, kwa kuwa hali hiyo imejitokeza, na siyo kutaka kwa shirika la uchukuzi kwa njia ya anga RVA.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.